NGODAZ

moto moto news

Watoto 163 wanaotumikishwa waachiwa huru CAR

Watoto 163 wanaotumikishwa waachiwa huru CARKundi la wanamgambo wa kikristo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati la anti-Balaka limewaachilia huru watoto 163 waliokuwa wakitumikishwa na kundi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi liliyotoa kupitia mpango wa amani unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Watoto hao ni miongoni mwa watoto zaidi ya 6,000 wanaoaminika kuwa wamekuwa wakitumikishwa kufanya kazi duni zikiwemo za upishi na usafishaji au kutumiwa kama wapiganaji na makundi yanayobeba silaha nchini humo. Mohamed Malick Fall, afisa wa Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF lililosimamia zoezi la kuachiliwa huru watoto hao katika mji wa Batangafo huko kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema hatua hiyo ni ishara ya utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na viongozi wa makundi ya wanamgambo ikiwa ni sehemu ya mchakato wa amani na maridhiano. Ameongeza kuwa mamia ya watoto wengine wanatarajiwa kuachiliwa huru kabla ya kumalizika mwaka huu. Zaidi ya watoto 350 waliachiliwa huru na makundi yanayobeba silaha mnamo mwezi Mei. Kwengineko katika koloni hilo la zamani la Ufaransa mapigano mapya yamezuka  katika mkoa wa kati wa Bambari na kusababisha watu wapatao 10 kuuawa baada ya wanamgambo wa kikristo wa anti- Balaka kumuua kwa kumkata kichwa kijana wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 19…/
  (chanzo tehran radio)
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Chapisha Maoni