Kutoka Maktaba: Dkt John Pombe Magufuli akiwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Unknown 23:41 Add Comment Edit DR John Pombe Joseph Magufuli was born on October 29, 1959. He holds a PhD in Chemistry from University of Dar es Salaam. He has been a Mem... Read More
# HABARI DR. SLAA AFUNGUKA (ALIYOONGEA LIVE) Dr. katika hoteli ya Serena akiwa na walinzi wake 7, amefika na kuamua kuweka kila kitu wazi kuhusu ukimya wake. Soma hapo chini alichozungumza Slaa: Kila mtu ana kiu ya kusikia Dr Slaa anasema nini, sijawahi kuona waandishi wengi hivi Slaa: Wengi mnafahamu sina tabia ya kuyumbishwa, ninasimami a lile ninaloamini, ijulikane kama binadamu sina chuki na mtu Slaa: Mimi sikuwa likizo kama mlivyoambiwa na wengine. Nimeamua kuachana na siasa tarehe 28 Julai 2015 saa 3 usiku. Naomba ijulikane kuwa nilishiriki majadiliano ya awali juu ya ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA, ila sikuafiki ujio wake. Slaa: Mchakato ndani ya CHADEMA ulianza mapema na jina langu lilipitishwa lakini bado sikuitangaza popote. Slaa: Suala la Msingi ni kuangalia kama ni ASSET au LIABILITY, ASSET kwa maana kwamba anakuja na watu wangapi kwenye chama Slaa: Tuliambia anakuja na wabunge wanaomaliza muda wao zaidi ya 50 na viongozi wengine toka CCM. Slaa: Siku zikapita sikupewa majina ya wabunge hao, wenyeviti wa CCM mikoa wala makatibu wakuu. Slaa: Upotoshwaji kwamba Dr Slaa alikubali toka mwanzo si kweli naomba viongozi wangu waseme kweli. Slaa: Kamati kuu tumekaa toka saa 9 hadi 12:30 kikao kikavunjika, ikasemwa iundwe kamati ndogo kunishawishi, nikakataa. Slaa: Niliandika barua ya kujizuru ndani ya kamati kuu kwa mwenyekiti wakati huo akiwa Profesa Safari, ambaye aliichana. Slaa: Mimi mwanasiasa niliyozoea naamini siasa ni sayansi haitaki uongo, haitaki udanganyifu. Slaa: Maamuzi yaliyofanywa, yalifanywa na mimi kwa ridhaa yangu mwenyewe. Slaa: Sisi katika familia yetu tumezoea propaganda hizo, nishasema kama mna ushahidi muulete Slaa: Nataka niwahakikishie D. Slaa na watoto wake wameendelea kula mihogo kama tulivyoahidi maana pesa imesaidia watanzania Slaa:Ni lazima mwanasiasa yoyote duniani hataji jina linachafuliwe, hata Dr Slaa hataki jina lake lichafuliwe ni haki yangu. Slaa: Jambo ambalo nataka nifafanue ni suala zima la LIABILITY au ASSET, ASSET nimelieleza, wamekuwa waongo hawakutekeleza Slaa: Mtu ambaye hata mwezi mmoja haujapita tangu useme CCM ikimteua Lowassa atajitoa, leo anasema ni msafi. Slaa: Wenyeviti waliokuja CHADEMA wote toka CCM ni mzigo, makapi. Slaa: CHADEMA inachukua mtu kwa sifa ya wizi wa kura, kama hatutaki kuiba kura sisi tunaenda kufanya Slaa: Suala la ASSET sikupata majibu, ndio maana hadi leo viongozi wangu wamepata kigugumizi, naongelea kwanini nimeondoka. Slaa: Mimi padri , yaani nikubali kuweka mkataba na shetani kwaajili ya kuiondoa CCM? unaondoa CCM kwa 'progamu series Slaa: Watu waliikubali CHADEMA kwaajili ya misingi ya uadilifu, leo tuna unadilifu? Slaa: Duniani kote tuhuma zinatolewa na ni jukumu la serikali kutoa majibu. Kama watu hawajui siasa bora wakae kimya. Slaa: CCM siwezi kuwahurumia, hata Lowassa hapa alipofika ni kwakuwa CCM ilimlea. Slaa: Kama ukikuta choo cha kitanzania, ukapakua kilichoko ndani ya choo na kuweka chumbani kwako, ipi ni choo? Slaa: Mimi nilikuwepo 2008 wakati tunajadili RICHMOND tunapozungumza masuala hayo ni kwakuwa tunayajua na tuliyaishi Bungeni Slaa: Lowassa tunamtuhumu mengi , mimi simtuhumu kwa RICHMOND tu, 2010 mimi nilimwambia atumbie hadharani RICHMOND ya nani Slaa: Ni afadhali nipotee kwenye siasa Tanzania na duniani kote kuliko kuyumbishwa na misimamo yangu. Slaa: Mimi nimeletewa rushwa asubuhi, nikamuuliza aliyeleta kama mimi unanipa milioni 500 unazo ngapi? Slaa: Mwanzo wa RICHMOND lazima urudi kwanza kwenye taarifa ya baraza la mawaziri februari, 2006. Slaa: Naomba mtambue kwamba suala hili la RICHMOND halikuanzia kwa Kikwete bali lilianzia kwa Mkapa. Slaa: 2006 feb 10, Waziri mkuu alikuwa Lowassa, sasa leo unapokuja kunambia hakuhusika maanake nini? Slaa: Ripoti ya Mwakyembe alitoa option mbili, Waziri Mkuu ajipime au Bunge lijadili na kutoa uamuzi, akakimbilia kujiuzulu. Slaa: Lowassa dakika ya mwisho aliingilia, hakusaini yeye ila aliagiza personal assistance wake akasaini. Slaa: Watu wanauliza kwanini namsema Lowassa mwenyewe ni kwakuwa anagombea urais wa nchi. Slaa: Nendeni basi Monduli kwa Lowassa na Karatu mlinganishe wakati nikiwa mbunge, halafu tuone huyu mnayemuita mtendaji. Slaa: Mnasema habari za shule ya kata, hizi sio zao lake ni upotoshwaji, aseme alibuni wapi wazo hili. Slaa: Ugomvi wangu na Masha ni kwasababu nilitoka hadharani na kusema Masha umeingilia mchakato wa serikali, nikawa adui. Slaa: Wakaandika uongo kuwa RICHMOND ni kampuni ya stationary wala sio umeme Slaa: Waziri Mkuu anajua yote halafu ananyamaza, kama alikuwa hajui ni mzembe, kama ni mzembe hafai tena kuwa Rais wa nchi. Slaa: Kumbuka Tanesco ni chombo kinachojitegemea, ikaagizwa kusaini mkataba ambao haikujadili, maanake ni nini? Slaa: CHADEMA tumaini jipya lilijengekea, vijana wanaliamini ninaogopa, kwa masikitiko ninasema sitaki baadaye tufike pabaya Slaa: Kama CHADEMA leo inafika hatua ya kujaza uwanjani watu kwa mabasi halafu mnasema kuna mafuriko,siko tayari kuwa zezeta Slaa: Udanganyifu huu wa kujaza watu kwa kubebwa na magari kuja uwanjani wakajaza uwanja walikuwa nao CCM Slaa: Nimewasikia CHADEMA jangwani, waliyoongea ni sehemu kubwa ya ilani ambayo ilishaandaliwa zamani, hakuna kipya. Slaa: Kinachoniumiza ni sisi kuwa wabovu zaidi ya CCM. Slaa: Nataka Lowassa ajue kuwa tunajua, Scotland inatuandikia kuwa achunguzwe kwa paundi milioni 400 alizopeleka marekani. Slaa: Halafu wanasema nikizungumza eti nitaharibu sifa yangu, wacha iharibike. Slaa: Mimi nimefundishwa kukemea maovu. Slaa: Leo anakuja mtu hapa anatuambia nyamazeni? Mimi sitaki kuingia kwenye mambo ya akina babu seya. Slaa: Leo baadhi ya vyuo vinatumia kesi ya babu seya kufundishia kama kesi ya ulawiti halafu lowaasa anasema ataifuta Slaa: Nani aliyeagiza maaskari waingie na mbwa pale mwembe chai msikitini? Sumaye huyu huyu aliagiza. Slaa: Lowassa akili yake ipimwe, kesi ya ulawiti Rais hapaswi kuingilia, anaingilia uhuru wa mahakama Slaa: Ni afadhali kutokuwa na Rais wa aina hii, Rais ambaye anatumia udanganyifu kwakuwa watu hawajasoma hafai. Slaa: Waswahili wanasema ukiumwa na nyoka basi hata jani ulikimbie, inabidi tuhakikishe kwamba tunakuwa makini Slaa: Alipokuwa Waziri Mkuu haya matatizo yanayotokea leo hayakutokea? laa: Mtu aliyesababisha migogoro ya mipaka halafu leo anataka kuwa Rais? Slaa: Wapo watakaosema ameichana CHADEMA, ameijenga CCM. Ukweli haugawanyiki, kama yameitandika CHADEMA ndio ukweli ulivyo Slaa: Nimesema sina chama ila mimi ni mtanzania, nitawatumikia watanzania kwa vipawa alivyonipa Mwenyezi Mungu. Slaa: Nimeombwa kugombea urais kwenye vyama vitano ila nimekataa kwakuwa mimi siamini katika kuhama hama vyama. Slaa: Mshenga niliyemtaja, alisema kanisa la kilutheri lote linamuunga mkono Lowassa, na maaskofu wa katoliki 30 wamehongwa Slaa: Sitaenda chama chochote, nimesema sina chama, siasa kwa maana ya chama sina, ila siasa kwa ninayoamini. Slaa: Sijaja kufanya kampeni leo, nimekuja kuwakumbusha Watanzania wasije wakajuta kama ambavyo tunajuta kwa kosa tulilofanya 2005 na 2010. Unknown 13:08 Add Comment Edit Docka slaa Read More
HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015 Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania wenzangu Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi. Mabadiliko ya kuondoa umaskini. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka Tusidanganyike, CCM hawana jipya Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi. Ndugu watanzania CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:- Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:- ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza. Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:- Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafi Unknown 12:42 Add Comment Edit Read More
Watoto 163 wanaotumikishwa waachiwa huru CAR Unknown 09:27 Add Comment Edit Kundi la wanamgambo wa kikristo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati la anti-Balaka limewaachilia huru watoto 163 waliokuwa wakitumikish... Read More