Rais wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji nchini humo
Sylvester Ambokile kupisha uchunguzi katika idara ya uhamiaji.
Taarifa
kutoka kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu Gerson Msigwa
imesema Bw Ambokile amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za rushwa,
ukusanyaji mbaya wa maduhuli ya serikali, ukiukwaji wa taratibu za
manunuzi na utendaji mbovu.Tuhuma hizo zilibainika wakati waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Charles Kitwanga alipotembelea idara ya uhamiaji hivi karibuni
Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bw Piniel Mgonja pia amesimamishwa kazi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema watendaji hao wakuu wa uhamiaji wamesimamishwa kazi mara moja hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
“Endapo watabainika kutokuwa na makosa Rais ataamua hatima yao,” amesema.
- Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa
- Magufuli amfuta kazi afisa mkuu wa reli
- Magufuli avunja bodi ya bandari Tanzania
Bw Maswi alikuwa ameteuliwa kuwa kaimu naibu kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
“Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo kwa lengo la kumtafuta mtu mwenye utaalamu wa kuendeleza kazi iliyofanywa na Bw Maswi,” Bw Sefue amenukuliwa katika taarifa hiyo kutoka ikulu.
Tangu kuchukua madaraka mwezi Novemba mwaka jana, Dkt Magufuli amewasimamisha au kuwafuta kazi maafisa wengi wakuu serikalini.
0 maoni:
Chapisha Maoni