Baraza la uhusiano mwema la kiislamu
nchini Marekani limemtaka mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump, kuomba msamaha kwa kuamrisha
mwanamke wa dini ya kislamu kufurushwa kutoka kwa mkutano wake wa
kisiasa.
Rose Hamid alilalamikia wito wa bwana Trump wa kuweka marufuku ya muda kwa waislamu wanoingia nchini Marekani.Bi Hamid mwenye umri wa miaka 56 na ambaye anafanya kazi ya huduma katika kampuni ya moja ya ndege ,baadaye aliamrishwa na afisa mmoja wa usalama kuondoka.
Alizomwa wakati alipokuwa akifurushwa katika mkutano huo.
Wafuasi wa Trump walipoketi, mwanamke huyo alisimama kwa ukimya, huku akivalia vazi lililokuwa na maandishi, salaam. Nimekuja kwa amani.
0 maoni:
Chapisha Maoni